Sambaza....

Kamati ya utendaji ya TFF imemteua aliyewahi kuwa kocha wa Ngorongoro Heroes na Timu ya taifa ya Tanzania bara “Kilimanjaro Stars” kuwa mkurugenzi wa ufundi wa TFF.

Amy Ninje anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Oscar Milambo ambaye alikuwa anakaimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi wa TFF Mzee Salum Madadi kuwa mwenyekiti wa mashindano ya TFF.

Kwa sasa Oscar Milambo anabaki kuwa Mkurugenzi wa soka la vijana , nafasi ambayo ilikuwa chini ya kocha Kimi Paulsen.

Kwa maana hiyo Amy Ninje atakuwa “boss” wa makocha wote wa timu zote za Taifa za mpira wa miguu akiwemo Kocha Emmanuel Amunike wa timu ya Taifa Stars.

Baadhi ya majukumu ya mkurugenzi wa Ufundi:

-Ni kuratibu na kusimamia maendelo ya mpira wa miguu.

– Kutengeneza mfumo maalumu wa mpira wa miguu ambao utakuwa rasmi kwa ajili ya mpira wetu.

-Makocha wote wa timu za taifa za mpira wa miguu watakuwa wanareport kwake kwa ajili ya kuwasilisha maendeleo ya timu husika za taifa.

Sambaza....