Wakati ripoti ya Singida United ikisema wachezaji waliojiweka kando klabuni hapo kwa madai ya kimaslai watarejea kuendelea na majukumu yao, mlinzi wa pembeni raia wa Uganda, Shafiq amejiunga na mabingwa mara nne mfululizo wa Kenya- Gor Mahia FC.
Wakati mlinzi huyo bora wa kushoto katika ligi kuu Tanzania Bara msimu uliopita akisaini miaka miwili ‘Kogalo‘, golikipa Peter Manyika Jr ambaye pia alijiondoa Singida United hivi karibuni anakaribia kujisajili AFC Leopards-mahasimu wa Gor.