Sambaza....

Bayern Munich wanaonekana ni vibonde kwa miaka ya hivi karibuni dhidi ya Real Madrid, katika michezo 6 ya hatua ya mtoano wamepoteza yote hii ni idadi kubwa kwao dhidi ya timu moja katika Uefa champions league

Bayern Munich, katika michezo yao 13, ya hivi karibuni ya Uefa champions league wakiwa ugenini wameruhusu nyavu zao kutikiswa

Bayern Munich, wamekuwa na rekodi nzuri na siku ya Mei 1 ikicheza mara mbili dhidi ya timu za Hispania na kushinda yote, Mei 1, 2001 Bayern Munich 1-0 Real Madrid na Mei 1, 2013 Bayern Munich 3-0 Barcelona

Image result for Santiago Bernabeu

Hakuna timu zilizokutana mara nyingi kunako michuano ya Ulaya, kama Real Madrid na Bayern Munich jumla ya michezo 26, wamekutana hadi sasa Real Madrid wakishinda michezi 12, huku Bayern Munich wakishinda michezo 11

Katika michezo ya nusu fainali 7 iliyopita hakuna timu iliyomudu kubadilisha matokeo, baada ya kufungwa kwa mabao 2-1 wakiwa kunako uwanja wao wa nyumbani.

Image result for bayern munich vs real madrid

Santiago Bernabeu bado ni mahali salama kwa Real Madrid, kunako michuano ya Uefa Champions League hii ni kufuatia kufunga jumla ya michezo 41, ya mwisho huku mchezo pekee ambao walipoteza ni dhidi ya Barcelona mnamo mwaka 2011

Sambaza....