Sambaza....

KIUNGO- mshambulizi wa Yanga SC, Ibrahim Ajib amewataka mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu kuacha kulaumiana kutokana na matokeo ya 4-3 dhidi ya Stand United.

Mashabiki wengi wa mabingwa hao mara 27 wa kihistoria wamekuwa wakilaumu namna safu yao ya ulinzi ilivyocheza, uku wakimtupia lawama nyingi zaidi golikipa wao Mcongo, Klaus Kindoki aliyefungwa Hat Trick katika mchezo wake wa kwanza tu akiichezea Yanga.

Ajib ambaye alifunga goli la pili dakika ya 32 na kuifanya timu yake kuwa mbele 2-1 amesema: ゛ Hatupaswi kulaumiana kutokana na matokeo haya ( 4-3) kwani hata sisi ( wachezaji) hatujui kilichotoke.)

Ajib alipiga pasi tatu za magoli kwa Mrisho Ngassa aliyefunga goli l la kusawazisha dakika ya 21 kufuatia ‘muuaji‘ Alex Kitenge kuifungia Stand United goli la kuongoza dakika ya 15 . Mfungaji huyo wa goli la pili akamtengenezea Vicent Andrew goli la tatu dakika ya 35 na kisha lile la Deus Kaseke dakika ya 57 lililoifanya Yanga kuongoza 4-1, kabla ya mechi kumalizika kwa 4-3.

Sambaza....