Sambaza....

Baada ya kocha mkuu wa Yanga sc, George Lwandamina kutimka klabuni hapo taarifa zinasema kuwa hakuwa na maelewano mazuri kati yake na Katibu mkuu Charles Boniface Mkwasa “Master”

Taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kwamba, Mkwasa anataka kurejea kunako nafasi yake ya ukocha na kuachana na ile ya Katibu mkuu anayoendelea nayo sasa

Baada ya kuondoka kwa Lwandamina klabuni hapo, Kamati ya utendaji ya klabu hiyo imepanga kukutana leo baada ya mchezo dhidi ya Singida United

Akiongelea suala hilo, mjumbe wa kamati tendaji ya klabu hiyo Samuel Lukumay amesema kamati yao itakutana hii leo na kutoa tamko la klabu kuhusiana na kuondoka kwa Lwandamina

“George yupo Zambia kama nilivyokwambia na tutaliongelea leo kwenye kikao chetu kamati ya utendaji baada ya mchezo wetu na Singida United”

Aidha pia Lukumay, alisema bado wana matumaini makubwa ya kumrejesha Lwandamina klabuni hapo, kwa kuwa kocha huyo anayapenda sana maisha ya Tanzania

Lwandamina alijiunga na Yanga sc, katikati ya msimu uliopita na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom

Sambaza....