Sambaza....

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, ametangazwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi mwaka huu

Kocha Gareth Southgate, amemteua Kane kuchukuwa nafasi hiyo kufuatia kutoa mchango mkubwa kunako klabu yake msimu huu

Kane, ameteuliwa zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi mapema mwezi ujao

Nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson, na kiungo wa Tottenham Hotspur, Eric Dier, kwa nyakati tofauti waliwahi kuongoza kikosi cha Uingereza chini ya Southgate lakini safari hii chaguo limekwenda kwa Kane

Kane ataongoza kikosi hicho cha Uingereza, maarufu kama Simba watatu kunako michuano hiyo mikubwa kabisa inayotaraji kuanza mapema mwezi ujao nchini Urusi

Sambaza....