Sambaza....

Mshambuliaji wa mabingwa soka Tanzania bara Yanga sc, Obrey Chirwa, amefikisha idadi ya kuwa na kadi tatu za njano katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania

Mshambuliaji huyo tegemeo kunako kikosi cha Yanga kwa sasa, ataukosa mchezo ujao dhidi ya mahasimu wao katika soka la bongo Simba sc, unaotaraji kupigwa Aprili 29, 2018 kunako uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es salaam.

Chirwa raia wa Zambia, atakuwa anatumikia adhabu ya kuwa na kadi tatu za njano ambapo kwa mujibu wa kanuni za ligi mchezaji hukosa mchezo mmoja unaofatia wa ligi anapofikisha idadi ya kadi tatu za njano

Chirwa alifikisha idadi hiyo, kufuatia kuoneshwa kadi ya njano katika mchezo wa jana uliopigwa kunako dimba la Sokoine mjini Mbeya ambapo Yanga ilicheza dhidi ya Mbeya city

Sambaza....