EPL

Licha Ya Arsenal Kushinda, Bado Ina Mapungufu

Sambaza....

Jana tulishuhudia Pierre-Emirick Aubameyang akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Arsenal. Mechi hii Pierre-Emirick Aubameyang alifanikiwa kufunga goli akipokea pasi kutoka kwa Henrikh Mkhitaryan ambaye alitoa pasi tatu za magoli kwenye mechi hii.

Mechi hii Arsenal alicheza katika mfumo wa 4-2-3-1, mfumo ambao ulimwacha Pierre-Emirick Aubameyang kuwa mshambuliaji wa mwisho, huku akizungukwa na Iwobi , Ozil pamoja na Henrikh Mkhitaryan.

 

Ozil mara nyingi alikuwa anashuka chini katikati kuchukua mipira kutoka kwa Xhaka na Ramsey kisha kuisambaza kwa kina Iwobi ambaye alikuwa anatokea pembeni kushoto na Henrikh Mkhitaryan aliyekuwa anaingia katikati akitokea pembeni kulia.

Kipi kilimfanya Aaron Ramsey ang’are katika mchezo huu?

Hat-trick katika mchezo huu, hat-trick ambayo ilitokana na yeye kuwa huru, alikuwa huru kutembea popote mpira ulipokuwepo, alikuwa anashuka chini kukaba na kupanda juu kushambulia.

Uhuru huu wa Aaron Ramsey ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na ubovu wa safu ya ulinzi ya Everton ambayo ilikuwa inatengeneza uwazi mkubwa katika eneo lao la kujilinda. Goli la kwanza la Aaron Ramsey, walinzi wa Everton waliacha uwazi , uwazi ambao aliutumia Ramsey hata wakati anapokea mpira alijikuta yuko huru peke yake, vivo hivo hata goli la tatu kwake ambalo lilikuwa la tano kwa timu.

Ni sehemu sahihi kwa Henrikh Mkhitaryan?

Kwa mchezo wa jana ulikuwa mchezo sahihi na salama kwa Henrikh Mkhitaryan kwa sababu ulimpa nafasi kubwa ya yeye kuwa mbunifu. Hali iliyopelekea aweze kutengeneza nafasi tatu za magoli.

Je Arsenal ya jana ndiyo Arsenal inayotakiwa iwe kwenye ushindani?

Hapana, kwa sababu zifuatazo. Kwanza kipimo cha Everton siyo kipimo sahihi kwa sababu Everton walikuwa wabovu kwenye kujilinda na kushambulia ( haikuwa timu ya ushindani )

Pamoja na kwamba Everton walikuwa siyo washindani wa dhati kwa Arsenal lakini walitusaidia kutupa pungufu la Arsenal.

Pungufu ambalo ƙlinatengeneza sababu yangu ya pili. Pungufu hilo ni aina ambayo Arsenal inatumia kujilinda.

Arsenal inajilinda vibaya kuanzia eneo la kiungo wa kati wa kujilinda mpaka mabeki wao.

Hawana kiungo wa kujilinda ambaye ni dhabiti kuilinda safu ya ulinzi ya Arsenal.

Xhaka anaruhusu sana presha kubwa katika eneo la mabeki wa Arsenal.

Kama wakifanikiwa kupata kiungo wa kati wa kuzuia itakuwa na faida kwao.

Pili, wanaposhambuliwa mabeki wao wa kati wanatengeneza uwazi katika eneo la nyuma, kiasi kwamba wakikutana na timu ambayo inajua kutumia uwazi (space) unaotengenezwa na safu hii ya ulinzi ya Arsenal inaweza ikawa na hasara kubwa kwao.

Kwa hiyo, pamoja na kwamba wamewaongeza Henrikh Mkhitaryan pamoja na Pierre-Emirick Aubameyang katika kikosi chao kitu ambacho kinaonesha kuongeza uzito kwenye kikosi na morali ndani ya kikosi, lakini wanatakiwa wapate kiungo mzuri wa kati wa kuzuia, tangu aondoke Patrick Viera hawajawahi kuwa na kiungo mzuri eneo hili, pili wanatakiwa waongeze beki wa kati, umri wa Laurent unaenda na anaonekana kupunguza utulivu pamoja na umakini kadri muda unavyozidi kwenda.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x