Sambaza....

Wakati ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara ikielekea ukiongoni, hali imeendelea kuwa ngumu kwa kikosi cha Yanga SC, kufuatia kupoteza mchezo mwingine wa ligi hiyo jioni ya leo dhidi ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0

Kikosi hicho, kimevuna alama sufuri katika michezo yake miwili mfululizo kufuatia hapo awali kufungwa na Tanzania Prisons kwa mabao 2-0 kunako dimba la Sokoine mjini Mbeya

Mchezo wa leo, uliopigwa kunako dimba la Jamhuri mjini Morogoro ulishuhudiwa kiungo wa zamani wa Ruvu shooting na Yanga, Hassan Dilunga akiipatia Mtibwa bao hilo pekee katika dakika ya 82, kwa shuti kali na kuufanya mchezo huo umalizike kwa matokeo hayo

Yanga SC, inafikisha idadi ya kupoteza michezo minne ya ligi baada ya kufungwa na Mbao katika mzunguuko wa kwanza, kisha Simba, Prisons na leo dhidi ya Mtibwa Sugar

Pia ikifisha idadi ya michezo 7 bila ya kupata ushindi tangu kuondoka kwa aliyekuwa Kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina, mara ya kupata ushindi ilikuwa Aprili 7, 2018 walipoifunga Waleyta Dicha ya Ethiopia kwa mabao 2-0 ambapo baada ya mchezo huo Lwandamina alitimka kunako kikosi cha Yanga SC

Matokeo hayo, yanaibakiza Yanga katika nafasi ya tatu kwa alama zao 48, huku Mtibwa Sugar ikiendelea kujiimalisha katiaka nafasi ya sita kwa kufikisha alama 37, kunako jedwari la ligi hiyo

Sambaza....