Sambaza....

Kocha mkuu wa timu ya Tanzania, Salum Mayanga amekanusha vikali juu ya taarifa iliyosema kuwa yeye hakufanya uteuzi wa kikosi cha timu hiyo

Mara baada ya Stars kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 4-1 hapo jana, mapema Leo Asubuhi kulizuka taarifa inayoeleza kuwa Mayanga hakuhusika katika uteuzi wa kikosi

Mayanga amesema kuwa taarifa hiyo ina lengo la kuvuruga kikosi, huku akithibitisha kuwa yeye ndiye aliyehusika kuteua kikosi na msaidizi wake Hemed Morocco akimuachia jukumu la kukitangaza

“Taarifa inayozunguka mitandaoni kuwa sijachagua kikosi cha timu ya taifa sio sahihi ni upotoshaji wenye nia ya kutuvuruga, watu waache kupotosha umma mimi ndio nimechaguwa kikosi chote kilicho safiri kwenda Algeria na si vinginevyo, Kocha Hemed Morocco nilimuachia jukumu la kutangaza kikosi baada ya uteuzi wangu” alisema Kocha huyo

Sambaza....