Sambaza....

Timu ya taifa ya vijana ya chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes, imetupwa nje ya mbio za kuwania kufudhu kwa Fainali za U20, Afrika kufuatia kufungwa mabao 4-1 na wenyeji Mali kunako uwanja wa Omnisports Modibo Keita mjini Bamako

Matokeo hayo yanaashiria kuwa, Tanzania imetolewa katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kwenda Niger 2019, kwa jumla ya mabao 6-2 baada ya kujubali kichapo cha mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza Mei 13, 2018 uliopigwa kunako uwanja wa taifa Dar es salaam

Mali sasa inataraji kukutana na mshindi wa jumla, kati ya Cameroon na Uganda katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuelekea Niger 2019

Sambaza....