Sambaza....

Msambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amewasili leo nchini Algeria na kupeokelewa na balozi wa Tanzania nchini humo Ndugu Omar Yusuf Mzee..

Mshambuliaji huyo yupo nchini humo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafika kati ya Taifa stars dhidi wenyeji Algeria utakaopigwa Machi 22, 2018

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Tanzania, anataraji kuungana na wenzake walioondoka leo nchini kulelekea Algeria tayari kwa mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki.

Samatta anayekipiga kunako klabu ya KRC Genk ya nchini Ubeligiji, ameitumikia klabu hiyo katika mchezo miwili ya ligi ya nchi hiyo baada ya kuwa nje ya uwanja kwa takribani majuma kadhaa akiuguza majeraha.

Sambaza....