Blog

Samue Samuel: Mawazo yangu juu ya Soka Letu

Sambaza....

Mohamed Rashidi wa Tanzania Prisons ana goli 6 ligi kuu katika michezo 11 lakini humuoni si Taifa Stars au Kilimanjaro Stars.

Kushindwa kuthamini changamoto ya vijana wengine nje ya Simba, Yanga , Azam na wachezaji wa nje ni jambo lingine linaloturudisha nyuma.

Vijana hawa tungekuwa tunawaweka katika mizani sawa na wachezaji wetu ‘ pendwa ‘ toka timu pendwa tungeweza kujenga saikolojia nzuri ya ushindani kuichezea timu ya taifa na mwisho wa siku kuleta tija na ufanisi.

Timu ya taifa kwa maana ya wachezaji angalau 28 kwenye note book ya mwalimu lazima wawe ni wachezaji wenye uwezo mkubwa kwenye ligi kuu au ligi daraja la kwanza . Nje ya hao 28 mwalimu anaweza kuwa na ‘ pool ‘ nyingine ya wachezaji angalau 20 ambao atakuwa yeye na jopo lake la ufundi akifuatilia uwezo wao mara kwa mara kama replacement kwa wale 28 endapo kuna kuumia au kushuka kwa kiwango.

Timu ya taifa si sehemu ya majaribio, ni sehemu inayotoa taswira ya soka la nchi. Tutambue timu ya taifa ina mashindano machache sana kwa mwako hivyo kama kila siku tutakuwa tunajaribu hatutafikia malengo kutokana na muda kusonga mbele.

Lazima tujitathimini kwanini tunakosa angalau wachezaji 20 wenye consistency nzuri na timu ya taifa kuanzia ngazi zote . Wachezaji wenye uwezo wa kukaa na timu za taifa kwa takribani miaka 8-10 !. Kwetu sisi imekuwa ngekewa mtu kuitwa timu ya taifa .

Tukiwa na mfumo mzuri , kila mchezaji atakuwa na hamu ya kuichezea hii timu kwa moyo wote na uzalendo uliotukuka.

Mbali na wachezaji lakini pia tuwe na tathimini nzuri kwa waalimu tunaowakabidhi hizi timu. Waalimu wenye uwezo mpana kusimamia mission zetu kisoka , kutuvusha kutoka hatua moja kwenda nyingine sio kuturudisha nyuma zaidi ya pale tulipokuwepo.

SAMUEL SAMUEL

Sambaza....