Mabingwa Ulaya

Spurs yawangojea Juve waje machinjioni tu!

Sambaza....

Hakika ulikuwa ni mchezo mzuri sana, wakuvutia na uliojaa ushindani mkubwa kutokana na namna ambavyo timu zilivyocheza, uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na matumizi ya mbinu kitimu ni vitu ambavyo viliingeza ugumu kwenye mchezo huuMIFUMO;

Juventus waliingia katika mchezo huu wakitumia mfumo wao wa 4-3-3 flat, kwa maana ya Giorgio Chiellin na Medhi Benatia kama walinzi wa kati huku Alex Sandro na Matia De Sciglio wakisimama kama walinzi wa pembeni, Sami Khedira, Miralem Pjanic na Federico Bernardeschi hawa walisimama kwenye eneo kiungo na ile flame ya juu ilikuwa na Mario Mandzukic, Douglas Costa na Gonzalo Huguain

Kwa upende wa Tottenham waliingia uwanjani wakitumia mfumo wa 4-2-3-1 kwa maana ya Ben Davies na Serge Aurier kama walinzi wa pembeni huku Davinson Sanchez na Jan Vertonghen kama walinzi wa kati, Moussa Dembele na Erick Dier wakicheza pamoja Double pivot, Erik Lamela, Dele Alli na Christian Eriksen hawa walicheza juu kidogo kuhakikisha wanasaidia kuzuia huku wakipandisha mashambuliza ya timu kumilisha mipira Harry Kane aliyecheza kama Target man

KIMBINU NA KIUFUNDI

Juventus licha ya kulazimishwa sare wakiwa nyumbani lakini walicheza vizuri kutokana na aina yao ya uchezaji, kwa maana upozungumzia soka la Italy tambua unazungumza namna gani timu inaweza kujilinda na mbinu za mpinzani wake

Game plan yao ilikuwa nzuri, kwa maana ya kufanikiwa kupata mabao mawili ya haraka lakini matatizo kwenye eneo kiungo kwa maana ya kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu ambao ulipelekea kucheza wachache kwenye eneo hili na kukubali kuirudisha timu chini huku wakishindwa kumiliki mpira hii sehemu kwanza iliyochangia kushindwa kulinda matokeo

Kushindwa kufanya marking au pre marking sawasawa hasa kwenye highline, pressing yao wakati wa kukaba haikuwa nzuri sana kiasi cha kuwaruhusu Spurs kupanga mashambulizi yao kuanzia mwanzo mpaka mwisho hii ilipelekea mashambulizi kuifikia safu yake ya ulinzi

Tactical philosophy, high speed passes, pass combination na pressing tactics hawakuwa sawasawa

Kwenye counter attacking tactics, attacking run ili kupata attacking play walikuwa vizuri na mara nyingi waliisumbua safu ya ulinzi ya Spurs kwa aina hiyo ya mbinu

Tottenham hotspurs kwa hakika wamekuwa na muendelezo mzuri sana katika uchezaji wao, unapozungumzia ubora wa Spurs basi ni eneo lake la kiungo hii ni sehemu inayosimama kama moyo wa timu hii, huku kumiliki mpira ikiwa ni siraha yao kubwa

Matatizo kwenye safu ya ulinzi kwa kushindwa kujipanga kwa wakati, ilipekea kuruhusu mabao mawili ya mapema ambayo kwa kiasi fulani yaliharibu game plan yao

Kushinda vita kwenye eneo la kiungo, hii ndio sehemu iliyochangia kwa kiasi kikubwa kuweza kupata sare hii Erik Lamela, Dele Alli na Christian Eriksen namna ambavyo walikuwa wakishuka chini kufata mipira kwa Mousa Dembele na Eeick Dier hakika walikuwa na muunganiko mzuri sana wa kimbinu, na kuifanya timu kuwa na namba kubwa kwenye eneo la kiungo

Uwezo wa kujenga mashambulizi yanayohama kutoka box moja kwenda lingine kwa kasi, na muunganiko mzuri kwenye njia ya kati kuliwafanya Juventus kurudi chini na wao kutengeneza nafasi na kusawazisha mabao

Tactical philosophy, high-speed passes, pass combination, speed on the ball of pressing game, pressing tactics walifanya kwa ubora mkubwa sana

Counter attacking pressing na counter attacking finishing pia walikuwa vizuri unaweza kuona hata bao lao kwanza lilichangiwa na matumizi mazuri ya mbinu hizi

Nb kuelekea mchezo wa marejeano pale Wembley bado ni 50% kwa 50 kwa maana timu zote zimeonesha uwezo wa kutengeneza nafasi na kuzitumia huku pia zikiwa vizuri kwenye kutumia udhaifu wa mwenzake

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x