Ligi Kuu

Sure boy kuivaa Simba sc leo

Sambaza....

Kiungo mzoefu wa Azam fc Salumu Abubakar maarufu kama “Sure boy” huenda akawemo kwenye kikosi kitakachoivaa Simba sc leo jioni

Katika mchezo huo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, unaotaraji kupigwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam

Kiungo huyo alikosa mchezo dhidi ya Ndanda fc, akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Yanga sc, mchezo amboa Azam fc walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1

Akimzungumzia kiungo huyo hafsa habari wa wanarambaramba hao Jaffary Iddi Maganga alisema mchezaji anaweza kuwemo kwenye kikosi cha kesho

“Salum amemaliza adhabu na yupo fit kuelekea kwenye wa kesho, na huenda kocha akamtumia kwenye huo” alisema Maganga

Itakumbukwa timu hizo zilitoka sare tasa kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa ligi hiyo, uliofanyika Kumasi dimba la Azam complex Chamazi jijini Dar es salaam

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x