Ni kweli amejieleza na kujitetea sana na kusema alikua anaulizwa maswali yenye mtego na kujikuta akiongea vitu vingi vya Simba lakini sio kwa kukusudia
Kuhusu wachezaji ambao hawajafika aliwataja ni Chama , Kahata na Shiboub ambapo amedai kuwa kwa sasa wanafanya kila wawezalo ili kuhakikisha wachezaji hao wanawasili.
Simba walitoa ahadi kwa mashabiki wao siku ya Jumamosi yakumleta mchezaji mmoja kati yao walitajwa hapo ili kuungana na wachezaji wengine watakaoingia kambini Jumatano.
Nae msemaji wa klabu ya Simba hakusita kuisifia tovuti yao na kuzungumzia ni rekodi klabu yake hiyo kumilki tovuti katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.