Blog

Mimi siyo bonge tena , Yanga wajiandae-KICHUYA

Sambaza....

Moja ya wachezaji ambao walifanikiwa kuwaonea Yanga SC kwa kiasi kikubwa kwenye michezo ya ambayo ilikuwa inawakutanisha watani hao wa jadi ni Shiza Ramadhani Kichuya .

 

Huyu alikuwa anawaonea sana kila alipokuwa anakutana nao,  huyu ndiye ambaye alikuwa mchezaji ambaye alifunga goli kwa mpira wa kona ulioingia moja kwa moja.

Alikaa Simba SC , akauzwa kwenye ligi ya Misri , alikaa kwa kipindi cha mwaka mmoja , lakini baadaye msimu huu alirejea katika klabu yake ya zamani ya Simba SC , lakini alirejea akiwa mnene sana .

 

Akizungumza na mtandao huu , Shiza Ramadhani Kichuya amedai kuwa wakati yupo uarabuni alikuwa hafanyi mazoezi sana ndiyo maana alinenepa sana.

“Nilikuwa sifanyi mazoezi sana wakati nilipokuwepo Urabuni ndiyo maana nilinenepa sana , kwa sasa nafanya mazoezi sana , nimepungua unene , Yanga SC wajiandae”- alisema Shiza Ramadhani Kichuya


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.