Ditram Nchimbi akimkimbiza mlinzi wa Simba Tairone Santos
ASFC

Simba yapata pakulipia kisasi kwa Yanga

Sambaza kwa marafiki....

Michuano ya kombe la FA maarufu kama AzamSports Federation Cup leo wamecheza draw ya michuano hiyo kwa kuzihusisha timu nane zilizobaki ambazo ni Namungo fc, Sahare Allstar, Ndanda fc, Azam fc, Kagera Sugar, Alliance fc, Simba na Yanga.

Matokeo ya draw hiyo iliyochezeshwa leo saa tano asubuhi na kuonyeshwa mubashara na Azam tv haya hapa chini.

Matokeo ya draw ya robo fainali ya michuano ya ASFC!

Katika draw hiyo Simba na Yanga huenda zikakutana katika mchezo wa nusu fainali endapo watashinda mechi zao za robo fainali. Endapo Simba akimfunga Azam fc na Yanga wakimfunga Kagera Sugar basi nusu fainali itakua ni ya watoto wa Kariakoo wenyewe kwa wenyewe.

Ambapo kwa upande mwingine mshindi kati ya Ndanda na Sahare All Star atakutana mshindu kati ya Alliance fc na Namungo fc.

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz