Sven Vandebroeck
Blog

CLATOUS,KAHATA KUTUA WIKI IJAYO,SHARAAF BADO.

Sambaza....

Kocha mkuu mkuu wa klabu ya Simba Sc Sven Vandenbroeck ameweka wazi kuwa wachezaji Clatous Chama ambae yupo Zambia na Francis Kahata ambae yupo Kenya watatua nchini wiki ijayo huku Sharaaf Shiboub ambae yupo Sudan akiendelea kusubiri mipaka ya nchini kwao Sudan ifunguliwe

Sven amesema viungo hao nchi zao Zambia na Kenya zimeanza kulegeza vikwazo ikiwamo kufungua mipaka baada ya kufunga kutokana na mlipuko wa homa ya virusi vya corona wakati kwa upande wa Shiboub bado itakuwa ngumu.

Sven Vandebroek na Selemani Matola

 

“Tunategemea kuwa na Chama na Kahata kwenye mazoezi kuanzia wiki ijayo lakini Shiboub nadhani atachelelewa kwa sababu nchini kwao bado hawajapunguza vikwazo,” alisema Sven.

Kuhusu mazoezi kocha Sven amesema wachezaji wanaendelea vizuri na morali iko juu ikiwa ni siku ya tatu tangu walipoanza rasmi kujiandaa na kurejea kwa ligi.

Sven amesema wachezaji wengi walijitahidi kufuata programu za mazoezi alizowapa kipindi cha mapumziko ingawa si kwa asilimia 100.

“Kwa sasa tunafanya mazoezi kwa kipindi kimoja ambapo kwa sasa tunatafuta pumzi na stamina na wiki ijayo tutaingia hatua ya pili ya mazoezi. Wachezaji wanaendelea vizuri na hali zao wote ziko vizuri,” aliongeza Kocha Sven.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.