Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Masingisa akiwa na msemaji wa Simba Hajji Manara
Stori

Simba yazindua tovuti yake rasmi!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba leo imefanikiwa kuzindua tovuti rasmi ya klabu ambayo ilianza kufanyiwa kazi tangu January ya mwaka huu na kua tayari kwa matumizi kuanzia leo tarehe 23 ya mwezi wa tano.

Kupitia kwa mtendaji wake mkuu Senzo Masingisa akiwa na msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara pamoja na watendaji wengine wa idara ya habari na tehama wa klabu wamefanikiwa kutambulisha tovuti ya kwabu ambayo itakua inajulikana kwa www.simbasc.co.tz.

Klabu ya Simba ikishangilia ubingwa wa Ngao ya Jamii, ni miongoni mwa taarifa zitakazokua zinapatikana katika tovuti ya Simba.

Senzo Masingisa amesema kwasasa ukiwa popote duniani unaweza kupata habari rasmi za klabu historia ya klabu pamoja na vitu vyote vinavyohusiana na klabu.

“Mtu hata akiwa Cairo Misri ana uwezo wa kuingia mtandaoni na kupata habari au historia ya klabu kubwa Africa bila wasiwasi. Tulianza tangu mwanzoni mwa mwaka lakini sasa imekamilika tunashukuru kwa hiki. Sasa kila kitu kuhusu klabu utakipata katika www.simbasc.co.tz”

Miongoni mwa histroia zitakazopatikana katika tovuti ya Simba. Hii sio Manchester United, bali ni Klabu ya Simba ikiwa katika jezi za Man Utd

Nae msemaji wa klabu ya Simba hakusita kuisifia tovuti yao na kuzungumzia ni rekodi klabu yake hiyo kumilki tovuti katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Hajji Manara ” Tovuti hii itakua na lugha mbili yaani kiswahili na kiingereza, wale wenzangu namimi kama huelewi Kingereza lugha ya kiswahili itakuwepo na hii inatufanya kuweka rekodi ya kua klabu ya kwanza kua na tovuti yenye lugha¬† mbili Kiswahili na Kiingereza katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.”

 

Sambaza....