Jonathan Nahimana
Tetesi

KMC yamkomalia mlinda mlango wake!

Sambaza....

Mlinda mlango namba moja wa timu ya Taifa Burundi na wana “Kino Boys” KMC ameandika barua ya kujieleza na kuomba msamaha kwa klabu yake baada ya kutamka kua anatamani kuchezea klabu ya Simba siku moja.

Mwenyekiti wa bodi ya klabu ya KMC na Meya wa Manispaa wa Kinondoni Benjamini Sitta amekiri kupokea barua ya utetezi ya kipa huyo baada ya uongozi wa klabu ya KMC kumtaka ajieleze kutokana na kauli yake.

Jonathan Nahimana akishindwa kuuthibiti mpira wa Odilo Ighalo!

Benjamin Sitta ” Sisi kama uongozi wa klabu tulimtaka ajielezee kutokana na alichosema kuhusu kuitamani kuchezea klabu ya Simba.   Ni kweli amejieleza na kujitetea sana na kusema alikua anaulizwa maswali yenye mtego na kujikuta akiongea vitu vingi vya Simba lakini sio kwa kukusudia.

Tayari barua yake ipo na sisi uongozi hatujatoa majibu, lakini pia mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu hivyo baada ya hapo ndo tutajua kama tutamuongezea mkataba ama tutamuacha.”

Benjamin Sitta ameongea hayo katika kipindi cha michezo cha redio ya Wasafi fm.

Sambaza....