Sambaza....

Timu ya taifa ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17, ya Tanzania Serengeti boys, jioni ya leo imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati, CECAFA U17

Serengeti boys, imeingia hatua hiyo baada ya kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika kunako dimba la Muyinga nchini Burundi

Serengeti boys, inayofundishwa na kocha Oscar Milambo, ilifanya kazi ya ziada hadi kuibuka na ushindi huo baada kutoka nyuma kwa bao 1-0 na kuwachapa Wakenya hao mabao 2-1 ndani ya dakika 90

Mabao ya washindi yalifungwa na Jaffary Juma dakika ya 22, huku Kelvin Paul akipigilia msumali wa mwisho kunako dakika ya 62

Vijana hao Watanzania, wanataraji kukutana na mshindi wa nusu fainali nyingine ambapo Uganda watavaana na Somalia

Sambaza....