Sambaza....

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti boys, imepata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Sudan katika mchezo wa kombe la mataifa ya Afrika mashariki na kati CECAFA inayoendelea nchini Burundi

Kwa matokeo hayo, yanaifanya Serengeti boys kufuzu hatua ya nusu fainali kutokea kundi B ikiungana na Uganda, zote zikiwa na alama nne kila mmoja huku Sudan ikiaga michuano hiyo baada kupoteza michezo yao miwili

Itakumbukwa kuwa Zanzibar, ilikuwa miongoni mwa timu zinazounda kundi hilo lakini iliondolea baada ya kugundulika kuwa na wachezaji waliozidi umri

Katika mchezo huo uliopigwa kunako dimba la Muyinga, mabao ya Serengeti boys yalipachikwa kimiani na Alphonse Msanga aliyefunga mara mbili dakika ya tano na 59, Mustapha Nankunku dakika ya 26, Edson Mshirakandi dakika ya 28, Jaffar Mtoo dakika ya 78, Kelvin Paul dakika ya 84

Serengeti boys, imefikisha alama nne baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa Aprili 15, 2018 kwenda sare ya 1-1 dhidi ya Uganda

Sambaza....