Sambaza....

Mzunguuko wa kwanza wa ligi kuu ya soka Tanzania bara ulikamilika mwishoni mwa juma lililopita huku ukishudiwa na changamoto mbalambali.

Simba sc wao wameibuka vinara katika mzunguuko huo wa kwanza, jumla ya alama 35 wamekusanya na kwa hakika msimu huu kikosi chao kimesheheni wacheza nyota hii tofauti sana na misimu kadhaa iliyopita ambapo walikuwa na wachezaji wengi vijana, pamoja na kumfuta kazi kocha Joseph Omog lakini hawakuwa na mwenendo mbaya

Azam Fc, hawa walikifanyia mabadiliko kikosi chao ambapo baadhi ya mastaa waliruhusiwa kuondoka na nafasi zao kuzibwa na vijana ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho, wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kujikusanyia alama 31, mwanzoni mwa msimu watu wengi hawakuwa wakiwapa nafasi kubwa lakini walichokionesha katika nusu msimu ni wazi kwa sasa ni kati timu zinazopewa nafasi kubwa ya kushinda taji la ligi kuu.

Mabingwa watetezi Yanga sc, wakionekana kuanza ligi hiyo kwa kusuasua huku hali uchumi klabuni hapo ikitajwa kama ni tatizo lakini pia majeruhi ya mara kwa mara kwa wachezaji wake tegemezi imekuwa ikiathiri safari ya kikosi hicho, bado wananafasi ya kutetea ubingwa wao kwa maana wanashika nafasi ya tatu kwa alama zao 28, hivyo katika mzunguuko wa pili lolote linaweza kutokea kwao.

Singida United hawa wamepanda msimu huu kunako ligi kuu, lakini kwa aina ya usajili uliofanyika na uwepo wa kocha mwenye uzoefu mkubwa na ligi ya Tanzania, Hans Van Der Pluijm wameonesha ushindani mkubwa na bado ni timu yenye nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi wapo nafasi ya nne wakiwa na alama 27.

 

Ukiachilia mbali na vilabu hivyo vilivyopigana vikumbo kwenye nafasi nne za juu, pia kuna vilabu vya Mtibwa sugar, Tanzania Prisons, Lipuli Fc, Ndanda Fc, Mbao Fc na Mwadui Fc hivi kwa pamoja vimeunda ile mid table na kwa hakika vimeleta changamoto kubwa kwa zile timu nne za juu, pia tutarajie hali hiyo na katika mzunguuko wa pili.

Lakini pia zipo zile zinazounda sehemu ya chini ya msimamo wa ligi hiyo, ambazo kwa namna ama nyingine mwenendo wao haukuwa mzuri kunako mzunguuko wa kwanza.

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2041394619401122279463
2Yanga SC1961334320326117209442
3Azam FC1981105038301148153380
4Tanzania Prisons196577267171190-19243
5Kagera Sugar FC189556371156198-42228

Mbeya City, tumeshudia wakifanya mabadiliko kwenye bechi lao la ufundi Kinnah Phiri akimpisha Ramadhani Nswanzirano, lakini bado mwenendo wao haukuweza kubadilika sana pengine muda ukihitajika zaidi kwa kocha Nswanzirano katika kuinusuru klabu hiyo isitelemke daraja.

Ruvu Shooting hawa walianza ligi kwa kipigo cha mabao 7-0 kutoka kwa Simba sc, mbali na kipigo pia mwenendo wao haukuwa mzuri kwenye mzunguuko wa kwanza, ni wazi wanahitaji kuboresha mbinu zao ili kujiweka kwenye mazingira mazuri.

Kagera sugar ni tofauti na misimu kadhaa iliyopita, ambapo wamekuwa na kawaida kuleta ushindani mkubwa lakini msimu huu hawakuanza vizuri pengine hata maandalizi yao hayakuwa mazuri  sana kama ambavyo wamekuwa wakifanya, bado kocha Mecky Mexime anaweza akabadili mbinu zake tukashuhudia hali tofauti kwenye mzunguuko wa pili.

Majimaji, Njombe mji na Stand United hawa nao kwa hakika kazi ya ziada inahitajika kuweza kujiweka katika nafasi nzuri.

Njombe mji bado inaonekana kuathiriwa na aina ya usajili uliofanywa kwenye kikosi hicho, pengine wachezaji wenye uzoefu mkubwa na changamoto za ligi kuu walihitajika zaidi kwenye kikosi chao.

Lakini ukiachana na hali ya vikosi vyote vinavyounda ligi kuu ya soka Tanzania bara, pia wapo wachezaji ambao walikuwa na mchango mkubwa kwenye vikosi vyao na hapa nakuletea orodha ya kikosi bora cha mzunguuko wa kwanza wa ligi hiyo.

Golikipa ni Razack Abarola kutoka Azam Fc

Walinzi wa pembeni ni Erasto Nyoni kutoka Simba sc na Shafiq Batambuze kutoka Singida United

Walinzi wa kati ni Yakub Mohammed kutoka Azam Fc na Asante Kwasi kutoka Simba sc

Viungo wa kati ni Papy Tshitshimbi kutoka Yanga na Stephen Kingu kutoka Azam Fc

Viungo wa pembeni ni Shiza kichuya na Emmanuel Okwi kutoka Simba sc

Washambuliaji ni John Bocco kutoka Simba sc na Ibrahim Ajib kutoka Yanga sc

Sambaza....