Sambaza....

HABARI ikufikie kwamba, nahodha wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameingia katika ‘rada’ za klabu tatu kutoka ligi kuu England. Everton ilikuwa timu ya kwanza kumtazama, Samagoal10, Burnley na sasa kocha wa zamani wa Machester City, Mchile, Manuel Pellegrini anamuhitaji kinara huyo wa magoli katika ligi kuu Ubelgiji kuungana na Marco Amautovic katika safu ya mashambulizi ya West Ham United.

Samatta ameanza msimu huu kwa kasi katika ufungaji, akifunga jumla ya magoli 14 hadi sasa- magoli saba katika ligi ya ulaya na mengine saba katika ligi kuu Ubelgiji ambako klabu yake ya KRC Genk inashika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa watetezi Club Brugge.

Vyanzo mbalimbali nchini England vimekuwa vikimuhisha nahodha huyo wa Taifa Stars kujiunga na ligi hiyo inayofuatiliwa zaidi na mara kadhaa Samatta amekuwa akisema hadharani kuwa ndoto yake ni kucheza England hata kama si klabu aishabikiayo-Manchester United.

Dirisha dogo la usajili mwezi Januari litashuhudia pilikapilika nyingio za wachezaji kuhama kutoka klabu moja hadi nyingine na baada ya dili lake la kwenda Levante ya La Liga na CSKA Moscow kukwama katika usajili uliopita mchezaji huyo bora wa Afrika mwaka 2015 kwa wachezaji wa ndani anaweza kuondoka Genk. Thamatta amepata thamani na huenda akauzwa kwa dau lisdilopungua pauni million tano.

Sambaza....