Sambaza....

Ni moja kati ya mechi nzuri ya kuvutia na iliyokuwa na ushindani wa kimbinu kwa pande zote, naweza nikasema timu zimeonesha kwa nini zipo nafasi za juu kunako msimamo wa ligi

Azam FC ambao wenyewe ndio walikuwa wenyeji wakicheza kwenye uwanja wao wa Azam complex, ambapo waliingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na rekodi ya kucheza michezo 14, bila kupoteza wakiwa wameweka kibindoni alama 30.

Katika mchezo wa leo wakitumia mfumo wa 3-5-2 ukiwaruhusu Himid Mao na Bruce Kangwa kupanda kwenye flanks na kuonekana kuisumbua Yanga, hapa Azam walikuwa bora kwenye tactical philosophy, pass combination, timing of overlapping na finishing a speed na haikushangaaza kupata bao la mapema sasa hapa ndipo makosa ya Azam FC yalipoanzia

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC2011374618394121273457
2Yanga SC1961334320326117209442
3Azam FC1981105038301148153380
4Tanzania Prisons193557266163184-21237
5Kagera Sugar FC187556270156197-41227

Azam walijitoa mchezoni licha ya kumiliki vema mpira na kuisumbua safu ya ulinzi ya Yanga, lakini hawakujua aina gani ya mipira ambayo ingeweza kuwasaidi kuongeza mabao zaidi matumizi ya high balls haikuwa sahihi kwao hasa ukizingatia aina ya washambuliaji wao

Safu ya kiungo ya Azam ilionekana kukosa ubunifu mkubwa mara walishindwa kujenga mashambulizi yao kupitia kati na kujikuta wakipiga square passes ambazo zilikosa madhara

Safu ya ulinzi ya Azam hakika kwenye mchezo wa leo walionekana kufanya makosa mengi, Agrey Morris na Yakub Mohammed walionekana kukosa muunganiko mzuri wa kimbinu kama central defenders, kushindwa kujipanga kwa wakati na kutofanya pre marking kulipelekea kuwapa nafasi sana washambuliaji wa Yanga na pengine wangekuwa makini wangeweza kuongeza bao

Razack Abalora hakuwa kwenye kiwango bora ambacho kimezoeleka, licha makosa ya safu yake ya ulinzi lakini ukitazama aina ya magoli aliyofungwa ukianzia la Chirwa alikosa umakini sawasawa na kujikuta anakubali kulambwa chenga goli la pili pia alikosa timing position na kujikuta anatoa nafasi kwa mfungaji

Kwa upande wa Yanga sc, wao walishuka dimbani mara 14 huku wakiwa wamepoteza mchezo mmoja wa ugenini dhidi ya Mbao FC na kuwa na alama zao 25

Wenyewe waliingia kwenye mchezo huu kama “underdog ” kutokana na mwenendo wao msimu huu na kuwakosa baadhi ya wachezaji wake nyota, na kwa hakika hii ilikuwa ni game plan nzuri sana kuitumia dhidi ya Azam

Wakitumia mfumo wa 4-3-3 huku wakionekana kumiliki eneo la kiungo hapa ndipo mahala walipotumia vema kuwamaliza Azam kwa tactical set up ya Makapu, Raphael Daud na Pappy Kabamba iliwafanya Yanga kujenga mashambulizi yao kwenye channels zote tatu yani katikati, kulia na kushoto

Yanga walikuwa bora sana kwenye attacking tactics, na uwepo wa watu kama Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib wakicheza pamoja kwenye flame ya juu hawa dedicated strikers ambao huitaji midfield na defense zone players kuiweka mipira kwenye advanced positions ili wao waifanyie kazi na ndio maana mara nyingi sana waliisumbua safu ya ulinzi ya Azam

Safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana kucheza kwa utulivu mkubwa sana, licha ya Azam kukosa mipango mizuri ya kushambuli lakini waliweza kujipanga kwa wakati na kuficha makosa ambayo yangeweza kuwapa nafasi Azam

Man to man defense system ilionekana kuisaidia sana safu ya ulinzi ya Yanga, Kelvin Yondan na Andrew Vicent wakiwa na muunganiko mzuri wa kimbinu kama mabeki wa kati

Hakika Yanga walistahili ushindi kutokana na ubora wa mbinu zao

Niseme tu kuwa Yanga walikuwa bora kwenye attempting position huku Azam walikuwa bora kwenye ball possession

Sambaza....