La Liga

Zinedine Yazid Zidane aweka rekodi mpya

Sambaza....

Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane, usiku wa jana katika mchezo wa Ligi kuu ya Hispania ameweza kuweka rekodi yake ya kushinda michezo 100, katika mashindano yote akiwa na Real Madrid

Zidane mbaye alitengeneza rekodi hiyo katika mchezo wa jana dhidi ya Malaga, ambapo Real Madrid waliweza kuishinda Malaga bao 2-1

Mabao hayo yalifungwa na Isco aliyefunga kwa faulo pamoja na Casemiro, Isco ambaye aliwahi kuichezea Malaga kabla ya kujiunga na Real Madrid.

Mpaka sasa Zidane ameiongoza Real Madrid kwa misimu mitatu katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na tayari ameshinda vikombe hivyo mara mbili mfululizo akiwa kocha wa klabu hiyo

Ushindi huo wa 100, kwa Zidane unamfanya kuwa kocha mwandamizi kuwahi kutokea katika ardhi ya Ufaransa katika kipindi kifupi akiwa kama kocha mkuu

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x