Sambaza....

Mshambuliaji wa Lipuli fc ya Iringa Adam Salamba ni rasmi sasa atajiunga na SimbaSc baada ya kukubali kusaini kandarasi na mabingwa hao wapya wa VPL.

Mshambuliaji huyo anaesifika kwa matumizi ya nguvu amejiunga na klabu ya Simba kwa  mkataba wa miaka miwili huku akizoa donge la milioni 40 kwa kusaini kandarasi na Wekundu wa Msimbazi.

Adam Salamba ambae alianza msimu huu akiwa na klabu ya Stand UTD ya Shinyanga kabla ya kuhamia Lipuli fc ya Iringa chini ya kocha Selemani Matola na nyota yake kung’aa kiasi cha kuwavutia vigogo wa mpira wa Tanzania Simba, Yanga na Azam kutaka kumsajili. Kabla ya Simba kufanikiwa kummbeba nyota huyo.

Adam Salamba akiitumikia Lipuli fc katika moja ya mechi za VPL.

Inaaminika kwamba kutokana na mahusiano mazuri kati ya Lipuli fc na SimbaSc ndio kwa kiasi kikubwa kimefanya mchezaji huyo aelekee Msimbazi badala ya Azam waliokua katika nafasi nzuri yakumsajili.

Adam Salamba anakwenda kuungana na John Bocco na Emmanuel okwi kwenda kuunda safu ya ushambilliaji huku pia akitegemewa kuungana na Marcel Boniventure Kaheza kutokea Majimaji katika kuimarisha safu ya Wekundu hão wa Msimbazi tayari kabisa kwa msimu ujao wa ligi na mashindano ya Kimataifa.

Sambaza....