Tahariri

Aheshimiwe mchezaji mzawa!

Sambaza....

Wakati taifa lenye ligi bora na pendwa zaidi Duniani ‘England’ likiendelea kuwapa nguvu, uwezo na kuwaheshimisha wachezaji wazawa, mambo yamekuwa tofauti Tanzania.

Mashabiki wa soka Bongo wengi hawaamini katika uwezo wa wazawa, hawataki wazawa wasajiliwe kwenye timu zao pendwa wanawataka wageni tu. Kibaya zaidi hawataki hata watambulishwe kwa heshima. (Ushamba)

Habibu Haji Kyombo akitambulishwa na Simba.

Mashabiki hao wanawahusudu wachezaji wa kigeni bila kujali namba, ubora na hitaji la timu zao, kila mgeni akija atasepa na kijiji hata kama ni galasa. (Mifano ipo)

Hakuna uzalendo tena, kila mmoja anajivunia mgeni kuliko mwanandinga mzawa na ukiwauliza utasikia “Hawa wabongo hamna kitu.” (Chuki)

Michael Sarpong akiitumia Yanga.

Utafikiri huyo anayesema maneno hayo sio mbongo. Hii inawaumiza sana wachezaji wazawa na kuwakatisha tamaa ya kupambana zaidi. (Liwalo na Liwe).

Maua wanayopewa kina Mayele, Sakho, Inonga, Mbombo, Bangala, Chama na Morrison ni tofauti kabisa na yale mnyauko wanayopata Mpole, Feitoto, Job, Kibu, Mzamiru, Bajana, Ndemla na Lusajo. (Mafundi).

Said Ndemla.

Kila shabiki haamini katika wazawa, sasa nani atawaamini? (Inafikirisha). 
Imagine hali hii ingekuwa mtaani kote na kumhusu kila mmoja nani angepona. (Hakuna)

Mfano wewe Daktari, Muuza Nguo, Mfanyabiashara, Mwalimu, Mchambuzi, Fundi, Dereva na yeyote yule nafasi hiyo uliyonayo ungenyang’anywa na kupewa mgeni ungejisikiaje? (Huzuni)

Bakari Mwamunyeto na Abdalah Shaibu “Ninja”

Au kwenye jukumu lako linalokuingizia kipato kungeletwa wageni mshindane kwa vigezo vya taaluma, ubora, na utendaji kazi unadhani watu/wateja wangekuwa upande wako? (Thubutuu).

Naam! Ukipata jibu la hapo badili mtazamo, wape nguvu, heshima na ushirikiano wazawa. Usiwavunje moyo kwani huko ndiko riziki yao ilipo. (Maisha)

Sambaza....