Sambaza....

Mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City, Eliud Ambokile, yupo safarini muda huu kuelekea Misri kwaajili ya majaribio karika klabu ya El Gouna SC inayoshiriko Ligi Kuu nchini humo.

Kwa mujibu wa ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo, taarifa zinasema klabu hiyo itaendelea kuwapa fursa wachezaji wake kwenda kufanya majaribio nje ya Nchi kwa lengo la kukuza vipaji vyao na mafanikio katika mpira wa miguu.

Mfungaji Bora mwezi wa Tisa wa ligi Kuu Tanzania bara, Eliud Ambokile, akiwa na zawadi yake kutoka katika tovuti ya kandanda ya kumpongeza.

Ambokile ameifungia klabu yake ya Mbeya City msimu huu bao 10.

Sambaza....