Sambaza....

Mshambuliajii hatari wa wagonga nyundo Mbeya City Eliud Ambokile “Aguero” anatimka kunako Africa ya Kaskazini katika nchi ya Misri kwenda kutafuta nafasi ya kusakata soka la kulipwa nchini humo.

Eliud Ambokile galacha wa mabao wa mwezi August anatarajiwa kuondoka leo usiku kuelekea nchini Misri ambapo haijawekwa wazi anaelekea katika klabu gani lakini pia haifahamiki anakwenda huko kwaajili ya kufanya majaribio au kusaini mkataba.

Afisa habari wa klabu ya soka ya Mbeya city amethibitisha hilo alipoongea na tovuti hii kuwa mfungaji wao bora mpaka sasa akiwa na mabao 11 katika TPL anaelekea nchini Misri.

“Ni kweli Eliud anaondoka leo usiku kuelekea nchini Misri na jana nilikua nafanya mpangilio wa safari yake. Mambo yakienda sawa leo hii atasafiri usiku.” Shah Mjanja alithibitisha.

Pia Shah Mjanja aliongeza “Anaelekea Misri lakini ni mapema kusema anaenda klabu gani na kufanya nini, taarifa zaidi zitawajia mambo yote yakishakamilika.”

Kwa miaka ya hivi karibuni Wachezaji wengi wa Tanzania wamekua wakielekea nchini Misri ili kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa. Yahya Zaid hivi karibuni amejiunga na Ismailia lakini pia Himid Mao pia yupo katika timu ya Petrojet tangy msimu umeanza.

Sambaza....