Kevin Kijiri "Kevin Nash" akiwa na Ally Ramadhani "Oviedo"
Tetesi

Beki KMC kwenda Kimataifa!

Sambaza....

Mlinzi mwandamizi katika klabu ya KMC Ally Ramadhani “Oviedo” huenda akaachana na  “Kino Boys” kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC, Kombe la FA na michuano ya Kimatafa.

Mpaka sasa Ally Ramdhani anaecheza mlinzi wa kushoto ni mchezaji huru baada ya kumalizika kwa mkataba wake KMC klabu aliyodumu nayo tangu Ligi daraja la kwanza.

Ally Ramadhani Oviedo akiwafungisha tela wachezaji wa Yanga, katika msimu wake wa mwanzoni akiitumikia KMC katika Ligi Kuu.

Kwa mujibu wa msimamizi wa mchezaji huyo Imani Mandu wamekiri wapo tayari kuokea ofa kutoka katika vilabu vingine vya Ligi Kuu au hata nje ya nchi kwani mpaka sasa  KMC wenyewe bado wapo kimya.

“Tupo tayari kupomea ofa kutoka klabu yoyote ya Ligi Kuu au hata nje ya nchi,” alisema

Kwa upande wa klabu yake aliyomaliza mkataba KMC wao mpaka sasa hawajatuma ofa yoyote.

Ally Ramadhani “Oviedo” akiwa mazoezini katika uwanja wa Bora Kijitonyama.

“KMC bado hawajawasiliana na mchezaji wala mimi msimamizi wake hivyo siwezi kusema moja kwa moja kua ataendelea kubaki KMC” Imani Mandu.

“Kikubwa tunaangalia sehemu ambayo atapata nafasi kubwa ya kucheza na tunatamani sana mchezaji aende sehemu ambayo atapata nafasi ya kucheza michezo ya Kimataifa maana kuna klabu nne zipo michuano ya CAF nchini kwasasa.” Alimalizia.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.