Kakolanya akiwa Taifa Stars
Tetesi

Benno Kakolanya nae kumfwata Kessy!

Sambaza....

Mlinda mlango mwenye mgogoro na klabu yake ya Yanga sc Benno Kakolanya huenda akatimka nchini na kuelekea nje ya nchi ili kusakata kabumbu.

Benno Kakolanya ameandika barua ya kuomba  kuvunja mkataba na klabu yake ya Yanga lakini mpaka sasa haijajibiwa na Yanga huku akiendelea kupokea stahiki zake za mshahara kama kawaida.

Tetesi zilizoifikia tovuti yako ya kandanda.co.tz ni kwamba “nyanda” huyo amepata timu nchini  Zambia na huenda wakati wowote ataondoka nchini akishapata majibu ya barua yake ya kuvunja mkataba.

Endelea kufuatilia tovuti hii ili kujua Benno anaelekea katika klabu gani ya nchini Zambia ambapo atakutana na Mtanzania Hassan Kessy anayeitumikia klabu ya Nkana Rangers.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.