Ni wazi Wanasimba wanategemea wachezaji wap kurudia kile kilichotokea miaka 20 nyuma yaani mwaka 2003 ambapo Mnyama alimtoa Zamalek ambae alikua bingwa mtetezi tena katika ardhi ya nyumbani kwake Misri
katika mchezo wa mwaka 2003 langoni alikaa Juma Kaseja na kwa ujasiri mkubwa aliivusha Simba kwa kudaka mikwaju ya penati baada ya matokeo ya sare kwa michezo yote miwili hivyo basi ni Benno ama Salim atapaswa kuvaa viatu vya Manula akiwa na ujasiri wa Kaseja
Kuelekea mchezo huo kumekua na sintofahamu ya hali ya afya ya wachezaji wake watatu ambao wamekosekana katika michezo ya hivi karibuni kutokana na majeruhi.
Kakolanya atakua katika majuto makubwa kwake na familia yake kwa kuigomea Yanga akishinikiza apewe stahiki zake lakini akikosa nafasi adimu na kuandika historia.