Ligi Kuu

Bocco awapiga chini kina Ngoma na Adam wa Prisons.

Sambaza....

Nahodha wa klabu ya Simba John Raphael Bocco “Adebayor” amefanikiwa kuibuka galacha wa mabao wa tovuti ya kandanda kwa mwezi Machi katika Ligi Kuu Bara.

John Bocco amefanikiwa kufunga mabao manne sawa na Adam Adam wa Tanzania Prisons na Donald Ngoma wa Azam fc. Lakini katika mwezi Machi John Bocco ameweza kuhusika katika michezo miwili tu ya klabu yake ya Simba huku Ngoma na Adam wakihusika katika michezo mitatu.

John Bocco alicheza michezo miwili dhidi ya Stand utd na Mbao huku akifunga mabao mawili kila mchezo na kuukosa mchezo mmoja dhidi ya Ruvu Shooting kutokana na kuwepo kambi ya timu ya Taifa.

Kwa magoli yake manne ndani ya mwezi Machi John Bocco tovuti ya Kandanda itasheherekea naye kwa kumpa zawadi yake kama ilivyo utaratibu wetu wa kusheherekea na Galacha wa mabao wa mwezi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.