John Raphael Bocco.
Uhamisho

Bocco ni mchezaji wa Simba na siyo Polikwane FC.

Sambaza....

Baada ya jana John Bocco kutangazwa kuongezewa mkataba na Simba, mkataba wa miaka miwili. Leo hii kiongozi wa Polikwane FC ya Afrika kusini amedai kuwa John Bocco alisajiliwa na Polikwane FC.

Akizungumza na EFM kiongozi huyo wa Polikwane FC amedai kuwa John Bocco ameshasajili na timu hiyo. Baada ya kugundua John Bocco amebakiza miezi 6 walizungumza na John Bocco na akasaini mkataba na Polikwane FC.

Mwenyekiti wa klabu ya Simba Sued Kwambi amedai kuwa haamini mchezaji wa kiwango cha John Bocco kama amesajili timu mbili.

Amedai kwa sasa yuko safarini lakini akirudi atakuwa na uhakika kama kweli John Bocco anaweza kusaini mkataba na timu mbili.

Mtendaji mkuu wa Simba alipotafutwa na EFM amedai kuwa Polikwane FC walikuja wakamsainisha mkataba wa awali (Pre-Contract).

John Bocco akiwa katika harakati za kutafuta ushindi nyumbani

“Walikuja Simba , wakamsainisha mchezaji kama Pre-Contract leo hii wameugeuza kama mkataba kamili, pamoja na kwamba John Bocco alikuwa amebakiza miezi 6 kwenye mkataba wake lakini walitakiwa kutuandikia barua”

“Hawakutuandikia barua ya kumtaka mchezaji na sisi tulipomuuliza John Bocco akadai kuwa hajasaini na Polikwane FC na sisi tukamsainisha” alidai Magori.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.