Barbar Gonzales
Uhamisho

Bosi Simba: Makocha Ulaya wanaitaka Simba

Sambaza....

Mtendaji mkuu wa klabu ya Simba Barbar Gonzalez amesema wamepokea CV nyingi kutoka kwa makocha wengi wakitaka nafasi ya kufundisha klabu ya Simba.

“Tumepokea wasifu wa makocha zaidi ya 100 kutoka sehemu mbalimbali duniani ambao wengi wao ni kutoka barani Ulaya na Amerika Kusini. Mchakato wa mchujo unaendelea na tunategemea utakamilika ndani ya wiki mbili zijazo,” Barabar Gonzalez.

Mohamed Adil Eradi kocha wa APR akitajwa kupigiwa hesabu na klabu ya Simba.

“Tunahitaji Kocha anayejua vizuri soka la Afrika pia tungefurahi kupata Kocha ambaye ni mzawa wa bara hili lakini mpaka sasa bado hawajatuma wasifu na aliteyuma mmoja na vigezo vyake havitoshi” Mtendaji wa Simba alisema.

Mapema baada ya kufungwa na Yanga katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la FA Simba ilimfuta kazi kocha wake Pablo Fanco aliejiunga na Simba Novemba mwaka jana kuchukua nafasi ya De Rossa.

Pablo Franco kibarua chake kimeota nyasi baada ya kushindwa kutetea vikombe viwili vya Ligi Kuu na FA lakini pia alishindwa kuifikisha timu hatua ya nusu katika Kombe la Shirikisho.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.