Tetesi

Coastal Union yaanza usajili na streka wa Azam fc.

Sambaza....

Wagosi wa Kaya kutoka jijini Tanga Coastal Union Fc wameanza mikakati ya kukiimarisha kikosi chao kwaajili ya msimu ujao kimyakimya huku wakianzia katika eneo la ushambuliaji ambapo kwasasa limeonekana kupwaya kidogo.

Tangu kuondoka kwa Andrew Simchimba aliekua akiitumikia Coastal Union kwa mkopo akitokea Azam fc Coasta inawategemea Ayoub Lyanga na Shabani Idd katika eneo la ushambuliaji.

Kocha wa Coastal Union Juma Mgunda akiwa na mshambuliaji wa Mbao fc Waziri JNR.

Lakini kwa tetesi za chinichini Coastal wanamtolea macho mshambuliaji  Waziri Junior wa Mbao fc. Waziri anaitumikia Mbal fc ambayo haipo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na huenda ikashuka daraja kama itaendelea na mwendo wake wa sasa wakusuasua.

Waziri Junior mchezaji wa zamani wa Azam fc na Toto Africans mpaka sasa ana mabao nane katika Ligi Kuu Bara. Hakuna mshambuliaji wa Coastal mwenye idadi hiyo ya mabao mpaka sasa kwenye VPL. Mchezaji mwenye mabao mengi wa Coastal mpaka sasa ni Ayoub Lyanga mwenye mabao saba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.