Tetesi

Dilunga Amechangua Njia Sahihi Kuachana na Simba

Sambaza....

Nimeona picha za Hassan Dilunga “HD” akisaini mkataba wa kuitumikia JKT Tanzania iliyorudi Ligi Kuu tena. Amechagua timu nzuri na sahihi kwake katika nyakati hizi.

JKT Tanzania watampa mechi nyingi za kishindani Hassan Dilunga. Hii itamsaidia kumrudishia kiwango chake kabla ya kwenda katika majeraha.

JKT Tanzania ni timu sahihi sana. Dilunga hajacheza mechi za kishindani kwa msimu mzima, ni ngumu mchezaji wa hivi kuisaidia Simba SC iliyo kwenye presha ya kujiunda upya.

Hassan Dilunga (kushoto) akiwania mpira na Djuma Shaban kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje msimu mzima.

Nadhani tunaona alichokipitia Sawadogo mpaka leo tumeona “Thank you” yake palepale Simba. Pale JKT, Dilunga atapata dakika nyingi. Hatokuwa na presha kubwa. Atavumiliwa pia.

Katika mazingira haya ni rahisi mchezaji kurudisha “touch” yake, kabla kuwavutia tena wakubwa. Kila la kheri HD, Hassan Dilunga.

Hassan Dilunga alijiunga na Simba katika msimu wa 2018/2019 akitokea Mtibwa Sugar alikofanya vyema. HD alikua katika kile kizazi cha mafanikio  haswa katika mashindano ya Afrika akiwa na kina Chama, Kagere, Mugalu, Okwi. 

Sambaza....