ASFC

Habari njema kwa mashabiki wa Mnyama

Sambaza....

Habari nzuri kwa mashabiki wa SimbaSc kuelekea mchezo wao wa ligi dhidi ya Njombe Mji Ya Njombe katika harakati zao za kuwania ubingwa kiungo wao Jonas Mkude ameaza kufanya mazoezi baada ya jeraha lake la enka kupata nafuu.

Jonas Mkude aliumia mazoezini baada ya kugongana na Yasin Mdhamiru katika uwanja wa Bokkobeach Veteran na kuzua hofuu kwa mashabiki wa Simba waliokuwepo uwanjani hapo wakishuhudia mazoezi hayo.

Simba imeweka kambi ya muda mjini Iringa na kufanya mazoezi katika uwanja wa Samora. Kiungo huyo alionekana akiungana na wenzake kufanya mazoezi.

“Hali ya Mkude imeendelea kuimarika zaidi na zaidi, leo ameanzaa mazoezi mepesi na kikosi chetu. Hali yake kwa sasa ni nzuri na ameshaanza mazoezi.” Daktari wa Simba Dr. Yassin Gembe amesema.

Kiungo Jonas Mkude pia Jana ilikua ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa ambapo aliungana na wachezaji na viongozi wa Simba kusheherekeaa.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x