Blog

Hii ndio ZESCO United! rekodi, Historia na mataji hivi hapa.

Sambaza....

Baada ya kuwatoa Township Rollers ya Botswana katika michuano ya ligi ya mabingwa Afrika, klabu ya Yanga itakutana na miamba ya Zambia, ZESCO United inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, George Lwandamina.

ZESCO UNITED FOOTBALL CLUB hii ni miongoni mwa vilabu vinavoendeshwa kisasa inayopatikana nchini Zambia katika mji wa Ndola, mji ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini humo ukiitoa miji ya Kitwe na Lusaka, ukiwa na  zaidi ya wakazi laki 4 kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2010. Mji huu ni maarufu sana kwa biashara ya madini, na ndio mji wa pili kwa ubora wa miundombinu yake.

Jina ZESCO kwanza haliandikwi kwa herufi Ndogo kwa maana ni kifupisho cha Zambia Electricity Supply Corporation.  Kwa maana ya Shirika la umeme nchini Zambia kwa hapa Tanzania ni sawa na kuiita TANESCO. Jina la utani la klabu hii ni Timu ya Ziko, kwa maana ya timu ya dunia, au timu ya taifa wakimaanisha kuwa wao ni timu moja na iliyoshikamana.

Zesco ni miongoni mwa vilabu vikubwa nchini Zambia vinavyoshiriki ligi kuu nchini humo. Zesco ilianzishwa  January Mosi mwaka 1974. Hadi leo, Zesco  ni kama Yanga na Simba tu kwani bado inatumia uwanja wa taifa kama uwanja wake wa nyumbani.

Zesco inatumia  uwanja wa kwanza wa kisasa wa taifa unaofahamika kwa jina la Levy Mwanawasa , wenye uwezo wa kubeba watu elfu 49,800. Huu ni uwanja unaotumika kwa matukio mbalimbali ya kitaifa, kama ulivyo uwanja wa taifa kwa Mkapa. Ujenzi wa uwanja huu ulianza mwaka 2010, ukiwa chini ya ufadhili wa serikali ya china, kupitia kampuni kikandarasi ya Shanghai Construction Group na ulikamilika mwaka 2012, na mechi ya kwanza kupigwa ni mechi ya kufuzu kombe la dunia kati ya Zambia na Ghana, na matokeo Zambia iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

Jina la uwanja huu, ni jina la Rais wa Zambia Levy Mwanawasa aliyetumikia kiti hicho kuanzia mwaka 2002 hadi 2008.

Kabla ya uwanja huu kukamilika Zesco ilikuwa ikichezea katika uwanja wa Dan Hammarskjold, uliokuwa na uwezo wa kubeba watu elfu 18 pekee, m waka 2001 uwanja huo ulisitishwa matumizi yake ili kupisha ujenzi wake lakini hadi leo kiwanja hicho kipo  kama kilivyo bila kujua ujenzi utaendelea au la!

ZESCO inafundishwa na kocha George Lwandamina. Lwandamina ni miongoni mwa makocha wazawa wanaopewa heshima sana nchini Zambia. Lwandamina  alishawahi kuwa mchezaji wa kutegemewa katika nafasi ya ulinzi katika klabu ya Mufulira Wanderers, timu ya taifa, na hata kocha mkuu wa timu ya taifa.

Lwandamina baada ya kustaafu Soka aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa Wanderers mwaka 1995 kabla ya kuja kuwa kocha mkuu mwaka 1997 baada ya kwenda kupata mafunzo ya ukocha nchini Ujerumani. Baada ya hapo Lwandamina alifanya makubwa ikiwemo kuipeleka timu hiyo robo fainali  klabu bingwa Afrika kabla ya kutolewa na Zamalek ya Misri.

Kocha huyu ana historia kubwa nchini Zambia, kuanzia mwaka 1997 hadi sasa amevifundisha vilabu 8 tofauti tofauti, ikiwemo klabu ya Yanga mwaka 2016-18 kabla ya kurudi Zesco baada ya kuiacha mwaka 2015.

Lwandamina amechukua vikombe vingi akiwa na Zesco United mwaka 2014, na hata kubeba tuzo ya kocha bora wa mwaka 2014 na 15 mtawalia.

Kwamujibu wa mtandao wa football Bloody Hell, Lwandamina ndiye mwanasoka  namba mbili katika historia ya soka nchini Zambia kupewa heshima zaidi baada ya SAMUEL ZOOM NDHILOVU kwa sasa ni Marehemu aliyeirudisha timu ya Wanderers katika makali yake mwaka 1960 hadi 1969 akiweka rekodi ya kubeba mataji matano ndani ya miaka 9 pekee huku matatu akibeba mfululizo.

Samweli Zoom ndiye aliyepata tuzo ya mwanamichezo bora wa Zambia mwaka 1964, pia akipewa tuzo ya Uaminifu baada ya kukataa dili nono la kwenda Black Pool ya nchini Uingereza.

Hadi sasa, Zambia inajivunia makocha hawa wawili na ndio wanaotajwa kuwa ndio makocha bora zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Kwa Tanzania ni nani?

JEZI ZA ZESCO.

Tangu kuanzishwa kwake, kumekuwa na mabadiliko madogo kwa upande wa  jezi zake kama ilivyo kwa timu zingine duniani kote lakini Rangi zake za msingi  hubaki kama zilivyo.

Kiutamaduni, ZESCO huvaa jezi za machungwa wakiwa nyumbani, Kijani wakiwa Ugenini na Nyeupe ni rangi yao ya tatu.

MASHABIKI.

ZESCO ni miongoni mwa vilabu vyenye mashabiki wengi nchini Zambia, Afrika na duniani kwa ujumla. Mashabiki wa Zesco hujiita ZESCOLO, Timu ya Ziko wanaoongozwa na kauli mbiu inayosema “NI ZAIDI YA KLABU” iliyoasisiwa na mashabiki wa ZESCO kutoka Colombia.

Mashabiki wengi wa ZESCO wanapatikana katika miji yote yenye utajiri wa madini ya Coppa na sehemu nyingine ikiwemo mji mkuu wa Lusaka.

UTANI WA JADI.

Watani wa jadi wa ZESCO United ni Zanaco, Nkana Red Devils, Power Dynamos na NAPSA Stars.

MAFANIKIO.

Hadi sasa klabu hii ina jumla ya mataji 19, huku 7 yakiwa ni ya ligi kuu nchini nchini Zambia, mengine ni Copa Barclays, ngao ya jamii, Zambia Cup, Zambia Cocacola Cup na Zambia Division One.

Kwa upande wa kimataifa, ZESCO imeshiriki klabu bingwa  mara tano, huku mwaka 2016 wakiishia hatua ya nusu fainali, kabla ya mwaka 2018 kuishia hatua ya Makundi.

Katika upande wa shirikisho Afrika, ZESCO wameshiriki mara tatu, huku mwak 2017 wakiishia hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Hii ndio klabu ya kwanza nchini Zambia  kufuzu hatua ya makundi kombe la shirikisho, walifanya hivyo mwaka 2009.

ZESCO pia inaungana na vilabu vya Nkana Red Devils na Green Buffaloes kutowahi fungwa na klabu yoyote kutoka nje ya Zambia katika uwanja wake  wa nyumbani.

ZESCO pia ndio klabu ya kwanza ya Zambia katika karne hii ya 21, kuwahi kucheza na timu kutoka nje ya bara la  Ulaya, Zesco ilicheza na Zenit Saint Petrsburg ya Urusi kule  Abu Dhabi mwaka  2008.

Je Yanga watavunja rekodi ya ZESCO kuifunga nyumbani kwao?

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x