Ligi Kuu

Kagera Sugar kiboko ya Simba!

Sambaza kwa marafiki....

Timu ya soka ya Kagera Sugar imeonekana kuwa mmbabe wa kudumu wa klabu ya soka ya Simba sc baada ya leo tena kuwadondoshea kichapo katika uwanja wa Uhuru.

Kagera sugar imefanikiwa kuondoka na ushindi wa bao moja kwa sifuri katika dimba la Uhuru huku goli lao likitokana na kujifunga kwa nahodha Mohamed Hussein “Tshabalala” katika dakika ya 41.

Kagera Sugar imeendeleza historia nzuri mbele ya Simba baada ya kufanikiwa kuifunga Simba nje ndani msimu huu huku pia ikiwa mara ya tatu mfululizo.

Katika mchezo wa kwanza Kagera Sugar waliifunga Simba mbili kwa moja huku pia msimu uliopita wakiwafunga bao moja kwa sifuri mbele ya Rais John Magufuli

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.