Kagere kwenye moja ya mechi
Blog

Kagere apandishwa mzuka na Mashabiki.

Sambaza kwa marafiki....

Mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Rwanda, Meddie Kagere amefunguka mbele ya Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Manara kuwa, akiwaona mashabiki wa Simba wamejazana uwanjani hupatwa na mzuka na humpa ari ya kufunga zaidi.

Kuelekea katika mchezo wao wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Ud Do Songo ya Msumbiji unaotarajiwa kupigwa siku ya jumapili, Kagere amesema kuwa, nguvu ya wachezaji wa klabu ya Simba kufanya vizuri katika  mchezo huo inatarajiwa kutoka kwa mashabiki licha ya timu na wachezaji wote kujipanga vizuri kuhakikisha Simba inasonga mbele katika hatua ya kwanza ya mashindano hayo.

Katika mchezo wa awali, Simba ililazimishwa sare ya kutofungana ugenini, kwa sasa  inajipanga vyema kuhakikisha inapata matokea katika uwanja wa nyumbani.

Aidha, kwa upande wake Haji Manara amewataka mashabiki na wadau wa soka nchini kufurika kwa wingi katika uwanja wa taifa Siku ya jumapili saa kumi  za jioni kuipa hamasa timu hiyo kupiga hatua zaidi katika michuano yua kimataifa.

“kwetu mashabiki sio mchezaji wa 12 kama ulivyo msemo wa Kiswahili, bali ni mchezaji wa kila nafasi uwanjani, tunashinda, tuna kikosi bora lakini mashabiki wanachangia sana..”

“tunataka mashabiki mshabikie mwanzo mwisho, tusisubili hadi Shiboub apige mtu chenga, mashabiki tunaenda uwanjani kushabikia…”

Katika mchezo huo, tiketi zinatarajiwa kuuzwa kama ifuatavyo;

Mzunguuko – shilingi 5000

VIP B na C- Shilingi 15,000

VIP A- Shilingi 30,000

Platinum – Shilingi 100,000

Platinum Plus – Shilingi 150,000.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.