Sambaza....

Tovuti ya kandanda.co.tz iliendelea na utaratibu wake wa kusheherekea  pamoja na wachezaji wanaofunga magoli mengi ndani ya mwezi moja kwa kukabidhi zawadi kwa Meddie Kagere na Emmanuel Okwi kutoka klabu a Simba Sc.

Kagere alikuwa ni mchezaji wa kwanza kuwa galacha wa mabao mwezi agosti, alifunga mabao matatu (3). Kutokana na changamoto ndogo hatukuweza kumkabidhi zawadi. Mwezi Septemba alikuwa ni Ambokile Eliud kutoka klabu ya Mbeya City ambae alipewa pia.

Meddie Kagere akikabidhiwa zawadi yake

Meddie Kagere baada ya kupokea zawadi alikua na haya ya kusema “Zawadi ni nzuri sana, lakini sikutegemea kupata kitu kama hiki chá kusheherekea na nyinyi. Zawadi hii ni maalum kwangu na wachezaji wenzangu wa Simba. Ntajitahidi sana niweze kuongeza mabao ili nipate tena zawadi hii kutoka kwenu.”

Mwezi Oktoba ulikuwa mzuri zaidi kwa Okwi, ambae alifunga goli 7 pekee, na kuwa galacha wa magoli mwezi huo. Lakini kwa ujumla wa magoli ya msimu alikuwa ni Ambokile ambae alikusanya goli 8. Zawadi zaki zilipokelewa na meneja wa Simba, ndugu Abbas Ally.

Meneja wa klabu ya Simba, Abbas Ally, akipokea zawadi ya Okwi

Meneja wa Simba aliepokea zawadi kwa niaba ya Okwi alisema ” Nashukuru sana kwa zawadi hii, na naamini Okwi mwenyewe atafurahi sana kwa hiki alichokifanya na alichokipata kutoka kwenu.”

“Ni utaratibu wetu wa kusheherekea na wachezaji galacha wa mabao tutaendelea nao ili kuongeza chachu na motisha ya kufunga zaidi.” Alinukuliwa msimamizi wa kandanda.co.tz, Thomas Mselemu.

Unaweza kutazama mwenendo wa wafungaji magoli hapa pia.

Sambaza....