Mshabiki wa Tanzania wakishangilia
Mashindano

Killi Stars yaibukia Zanzibar

Sambaza....

Michuano ya Challenge imeendelea leo nchini  Uganda kwa kushuhudia ndugu wawili wakiumana katika dimba la KCCA katika mchezo wa pili wa kundi B.

Tanzania Bara baada ya kuanza vibaya michuano hiyo kwa kupoteza bao moja kwa sifuri dhidi ya Kenya, leo Killi Stars imeweza kuibuka na kuweka matumaini baada ya kuifunga Zanzibar Heores kwa bao moja kwa sifuri.

Bao pekee katika mchezo huo mkali na wa kusisimua limefungwa na mshambuliaji hatari sana kwa sasa Ditram Nchimbi baada ya Eliuta Mpepo  kumiminina “mtungi” uliomshinda mlinda mlango wa Zanzibar na kuuweka kimiani katika kipindi cha kwanza.

Ditram Nchimbi mfungaji wa goli la ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya Zanzibar Heroes.

Baada ya ushindi huo wa bao moja kwa sifuri ni kama Tanzania Bara wamelipiza kisasi kwa ndugu zao baada ya kufungwa kwa magoli mbili kwa moja na Zanziabar katika michuano hiyo iliyofanyika mwaka 2017 nchini Uganda.

Kwa matokeo hayo sasa Killi Stars inakua na alama tatu baada ya michezo miwili huku Zanzibar Heroes wakibaki na alama yao moja walioipata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Sudan.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.