Blog

Kiongozi Yanga: Simba imepigwa na mwekezaji

Sambaza....

Aliewahi kua katibu mkuu wa Yanga sc nyakati za nyuma amesema thamani halisi ya Simba sio bilioni ishirini kama ambavyo imekua ikisemwa na mwekezaji wa Simba Mohamed Dewji ambae anategemea kua mwekezaji katika klabu hiyo.

Dr Jonas Tiboroha alikua katibu mkuu wa Yanga kipindi cha Mwenyekiti Yusuph Manji amesema Simba ina thamani ya zaidi ya bilioni 200 na si bilioni 20 kama ambavyo Mohamed Dewji aliyotangaza kama thamani halisi ya Simba sc.

Mahomed Dewji akiwa na viongozi wengine wa Simba. Mo ndie mwekezaji katika klabu ya Simba ambapo anatarajiwa kumiliki asilimia 49 pindi ambapo mchakato ukikamilika.

Tiboroha “Simba ina thamani ya zaidi bilioni 200  kwasababu klabu haifanyiwi “valuation” kwa yale majengo tuu au uwanja, ni zaidi ya hapo Simba ina mtandao mkubwa katika jamii. Viongozi wa Simba ndio wameshindwa kujua thamani halisi ya Simba wala simlaumu Mo(Dewji) maana yeye sio kiongozi wa Simba.

Sasa kwa maana hiyo Simba imepigwa wale hawana hiyo thamani ya hiyo pesa. Hiyo bilioni 20 inaweza kua labda asimia tano tu ya uwekezaji.”

Dr Jonas Tiboroha ambae kitaaluma ni mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam ameongea hayo katika kipindi cha Sports Headquator kinachorushwa na redio ya Efm.

Sambaza....