Zamani

Kisanga cha Ferguson kumpiga na kiatu Beckham!

Sambaza....

Haina ubishi kwamba David Beckham alikuwa ni staa mkubwa ndani na nje ya uwanja miaka ile ya 2000. Kwa tunaomjua, punde unapolisikia jina la nyota huyu picha inakujia jinsi alivyokuwa mtaalamu wa kupiga ‘free-kicks’ akijipinda kama upinde.

Akiwa ni mmoja wa wachezaji wa Manchester Utd waliohitimu kutoka akademi ya klabu hiyo mwaka 1992, Beckham kwa malezi ni kama mtoto wa kocha Sir Alex Ferguson. Kama unamjua vizuri kipindi hicho Beckham alikuwa anapenda sana mitindo ya nywele iliyomuongezea mvuto na umaarufu, lakini kuna mitindo mingine kama Mohawk (Kiduku) ulimchukiza Ferguson. Mara kadhaa alimwambia anyoe, ilikuwa kabifu fulani, ila maisha yaliendelea japo kinafki.

David Beckam.

Kadri siku zilivyoenda Ferguson alianza kuona kuwa Beckham anajikuta mkubwa kuliko yeye. Fergie akawataarifu wajumbe wa bodi ya Utd kuwa msimamo wake ni uleule, kwamba ile dakika mchezaji anapojiona ni mkubwa kuliko kocha, lazima aondoke, kwani kocha anapopoteza mamlaka dhidi ya wachezaji basi hapo hakuna tena klabu na watamuendesha watakavyo.

Bifu lilikuja kuwa kali 15 Februari 2003 Man Utd ilipotolewa kwa goli 2-0 na wapinzani wao hatari Arsenal katika hatua ya raundi ya tano ya michuano ya kombe la FA. Ferguson alimlaumu wazi wazi Beckham kuwa ndiye aliyesababisha timu kufungwa kwa kucheza hovyo kwenye mechi hiyo.

Sir Alex Ferguson na David Beckam.

Wakiwa vyumba vya kubadilishia nguo, Ferguson akiwa mwenye hasira huku akifoka foka, alipiga kiatu (Njumu) kikatua kwenye jicho la Beckham na kumpasua. Beckham akahamaki na kunyanyuka ili amzingue babu Fergie, lakini wachezaji wakamzuia asimchape mzee wa mabigijii.

Baada ya tukio hilo mahusiano ya Beckham na Ferguson hayakuwa mazuri tena, Beckhama akaanza kukalia benchi hadi alipoondoka majira ya kiangazi mwaka huo wa 2003 alipojiunga na Real Madrid.

Sambaza....