Tetesi

Kiungo aliyeikataa YANGA, kutua SIMBA leo mchana!

Sambaza....

Tangu dirisha dogo la usajili lifunguliwe klabu ya Simba hajitangaza mchezaji yoyote ambaye wamemsajili zaidi ya kuwaona Yanga wakiendelea kusajili kwa tambo.

Leo hii msemaji mkuu wa Simba , Haji Manara amedai kuwa kuna wachezaji wawili ambao watawasili katika uwanja wa ndege kwa ajili ya kumalizana na Simba.

“Leo hii kuna wachezaji wawili wa kimataifa watatua katika uwanja wa ndege na Hashim Mbaga ataenda kuwapokea kwa ajili ya kumalizana na Simba, wenzetu wamesajili kwa mbwembwe sisi tumenyamaza tu”. Alidai msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mchezaji wa UD Songo , Luis Miquissinho ameandika kuwa atakuwa Dar es Salaam muda mfupi , mchezaji huyu aliwakataa Yanga ambao walikuja na dau dogo, yeye alikuwa anataka milioni 110 za kitanzania na inawezekana amekubaliana na Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.