Luis Miquisone
Blog

Kwenye Miquissone yupo Sakho kwenye Sakho hayupo Miquissone!

Sambaza....

Wengi watajiuliza nini maana yangu juu ya hao wachezaji waliocheza Simba kwa vipindi viwili tofauti kila moja akikonga nafsi za mashabiki wa Wanamsimbazi na wasio wa club hiyo.

Nilichogundua kwenye Miquissone unamapata Sakho ,kwenye Sakho unamkosa Miquissone

Sakho

Nimekuwa nikijaribu kufuatilia kwa kina aina ya uchezaji wa hawa jamaa ( Play style ) nakubali wanatofautiana kwa mbali sana na wanafanana kidogo sana

Achana na kufanana maumbo yao kwa asilimia kadhaa ( wadogo wadogo) ama ‘wachache’ kwa maana ya kukosa nyama
ambayo sifa kuu ya wachezaji wa hivi ni kushiba kwa vichwa vyao kwa maarifa ya mchezo ( skills) wana akili sana wana ushapu sana kasi ambayo ndiyo silaha yao kuwakwepea wapinzani au ‘maadui’ wenye maumbo makubwa

Luis Miquissone ni most gifted kuliko Sakho kwa maana ana kipaji kikubwa zaidi anachagizwa na hard work yake ndiyo maana anaweza kukupa kila kitu ambacho Sakho angekitoa kwa timu ama unaweza kusema ni Complet package ya player

Dribbling skills ,turn up ,Pace decision make up na hapa ndiyo kwenye ubora wa chinga wa Mozambique natakupa over 90% kwa usahihi mkubwa

Individual Ability always anaiconnect na timu kwa hiyo akifanya mambo yake binafsi zao la mwisho ( end product) lina faida kubwa kwa timu

Sakho yes yupo good ama’ tununu’ pace yake anaweza kubattle kabisa na Miquissone ball control basic movement nk ni ya kuvutia sana dribbling and running with a ball skills zipo poa haswa

Tatizo la kwanza ambalo linamtofautisha na Miquissone too much individuality hata kwenye sehemu ya kucheza kitimu ili mtoke kwenye eneo fulan end product mara nyingi si nzuri kwa kuwa haiji kwa muda usahihi

Footwork Miquissone 100% miguu yote kwa ufasaha mkubwa tofauti na Sakho only mguu wa kulia wa kushoto wakuvalia boxer (utani).

Wanachofanana kwa pamoja ni ufanyaji kazi wa homon yao ya Adrenal gland ambayo inampa binadamu ushujaaa na uwezo wa kukimbia kama kuna hatar ikiwemo kupambana na adui

Mchezaji mpira hii ikimtokea akiwa uwanjani unaweza ukaufuata ukuta wa walinzi hata kama wapo 100 ukapenetrate na kufunga kama vile goli lake Jana Luis alifunga goli gumu na Ahly

Sambaza....