La Liga

‘Maradona’ ajiunga na RCD Espanyol.

Sambaza....

Mshambuliaji matatawa timu ya Shanghai SIPG Wu Lei ‘Chinese Maradona’ amejiunga na klabu ya soka ya Espanyol inayoshiriki ligi kuu nchini Uhispania.

Lei mwenye umri wa miaka 27 na ambaye alipewa jina la Maradona wa Uchina kutokana na aina yake ya kucheza, amejiunga na timu hiyo ambayo ipo katika hali mbaya wakiwa katika nafasi ya 15 kwenye ligi yenye timu 20 na matumaini yao ni kuona anawasaidia ili kubaki kwenye ligi hiyo kwa msimu mwingine.

Akiwa katika ligi kuu nchini Uchina aliiwezesha klabu ya Shanghai SIPG kutwaa ubingwa msimu uliopita akifunga mabao 27 na pia kutwaa kiatu cha mfungaji bora.

“Lei ambaye ni mchezaji wetu mpya atavaa jezi namba 24,” amesema mmiliki wa klabu ya Espanyol Mchina Chen Yansheng ambaye pia amekataa kutaja kiwango cha uhamisho akisema kuwa “Ni jambo ambalo bado linafuatiliwa, SIPG wataendelea kufuata matakwa yote kwani kwa kuwa ni uhamisho lazima mchezaji na klabu wapate stahiki zao kwa maendeleo ya pamoja kati ya mchezaji na vilabu,”.

Espanyol wanatangaza usajili huo wakitoka kupokea kichapo cha mabao 2-4 kutoka kwa Real Madrid jana kwenye muendelezo wa ligi kuu nchini Uhispania (LaLiga).


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.